3 Machi 2015 - 20:35
Mkutano kuhusu mustakabali wa Palestina

Uongozi wa Palestina unakutana wiki hii kwa mazungumzo muhimu kuhusiana na hali ya baadaye ya mamlaka ya Palestina ,

Uongozi  wa  Palestina  unakutana  wiki  hii  kwa  mazungumzo muhimu  kuhusiana  na  hali  ya  baadaye  ya  mamlaka  ya Palestina , ambayo  uhai  wake  uko  hatarini  baada  ya  Israel kuzuwia  chanzo  muhimu cha  mapato.

Chama  cha  ukombozi  wa  palestina  PLO , kinachotambulika  kama mwakilishi  halali  wa  watu  wa  Palestina  pamoja  na  chombo chake  kinachotoa  maamuzi , vitajadili  masuala  kadhaa  ya dharura   ya  kiuchumi  na  kisiasa.

Mkutano  huo  wa  Ramallah  unaoanza  Jumatano  utaangalia  hali iliyopo  ya  dharura  ya  mzozo  wa  kifedha  unaikabili  mamlaka hiyo  ya  Palestina.

Katika  muda  wa  miezi miwili  iliyopita , Israel  imezuwia  mamia  ya mamilioni  ya  dola  kutokana  na mapato  ya  kodi  kwa  mamlaka hiyo, baada  ya  hatua  ya  Palestina  kujiunga  na  mahakama   ya kimataifa  ya  uhalifu  ili  kuishitaki  Israel  kwa  madai  ya  uhalifu  wa kivita.

Matatizo  ya  fedha  yamesababisha  mamlaka  ya  Palestina kushindwa  kuwalipa wafanyakazi  wake 180,000.

Israel ni ilichukua kwa nguvu ardhi za Palestina na kuwashambulia kwa silaha kali raia wa nchi hiyo na hatimaye kuwafanya kuwa dhaifu na kuwaacha katika hali ya umsikini wa hali ya juu.